Picha kwa hisani –
Hii leo Kenya inajiunga na mataifa mengine wanachama wa umoja wa mataifa kuadhimisha siku ya choo duniani.
Siku hii husherehekewa kila mwaka ifikapo tarehe 19 mwezi Novemba ili kueneza hamasa kwa watu bilioni 4.2 wanaoishi bila choo bora kote ulimwenguni.
Maadhimisho haya ni kuhusu kuchukua hatua ya kukabiliana na shida ya usafi wa mazingira ulimwenguni, na kufikia Lengo la Maendeleo Endelevu, maji na usafi wa mazingira kwa wote ifikapo mwaka 2030.
Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Usafi endelevu na mabadiliko ya hali ya hewa.