Story by: Mwahoka Mtsumi
Kenya imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya misitu.
Siku hii iliidhinishwa rasmi na baraza kuu la umoja wa mataifa mnamo mwaka 2012 ili kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kuidhinisha miradi ya kuongeza viwango vya misitu duniani ikiwemo kuendeleza upanzi wa miti.
Umoja wa mataifa hata hivyo umeeleza kwamba kila mwaka ulimwengu hupoteza jumla ya ekari milioni 10 za misitu, licha ya watu zaidi ya bilioni 1.6 kote ulimwenguni kutegemea misitu kwa chakula, kawi, dawa, kipato na makaazi.
Kwa upande wake Waziri wa Mazingira na misitu nchini Soipan Tuya, amewahimiza wakenya kukumbatia umuhimu wa kulinda mazingira, misitu pamoja na kujihusisha na upanzi wa miti ili kuisaidia serikali kufiakia azimio lake la kupanda miti bilioni 10.
Hata hivyo kauli mbiu ya mwaka huu ni Misitu na afya.