Story by Our Correspondents-
Rais William Ruto anatarajiwa kurejea nchini baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Korea Kusini.
Katika kikao na viongozi wakuu wa taifa hilo, Rais Ruto ameliomba bunge la Korea Kusini kupitisha sheria itakayorahisisha biashara kati ya Kenya na Korea kusini ili kuboresha zaidi uchumi wa nchi.
Rais Ruto amesema malengo ya serikali ya Kenya ni kuhakikisha inauza bidhaa za kilimo nje ya nchi na hatua hiyo itaafikiwa kupitia mikakati bora ambayo itafungua soko la Chai, Parachichi na kahawa.
Kiongozi wa taifa ameahidi kushirikiana na serikali ya Korea kusini kuimarisha maswala ya uzalishaji wa nisharti safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.