Story by Mwahoka Mtsumi –
Wizara ya Afya nchini imesema Kenya inajiandaa kusambaza dosi nyengine ya chanjo ya AstraZeneca kwa wananchi kuanzia mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa afya nchini Dkt Patrick Amoth, amesema hatua hiyo ni katika juhudi za kudhibiti msambao wa virusi vya Corona nchini kwani taifa tayari limeripoti kirusi kipya cha India.
Akizungumza katika kikao cha kila siku cha kutoa takwimu za maambukizi ya Corona, Dkt Amoth amesema ni vyema iwapo wakenya wataendelea kukumbatia mpango wa kuchanjwa ili kuzuia maambukizi zaidi.
Hata hivyo Wizara ya afya nchini imewahimiza wakenya kuendelea kuzingatia masharti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.