Mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa Tong-ILmoo-doo nchini Clarence Mwakio ameeleza imani yake kuwa timu ya taifa ya mchezo huo itahifadhi ubingwa wake kwenye makala ya sita ya Mombasa open Tong-Ilmoo-Doo International Championship yaliyoratibiwa kuanza rasmi tarehe nane mwezi ujao wa Septemba mjini Mombasa.
Mwakio amesema kuwa timu ya taifa ya kenya ya tong-ilmoo-doo imejiandaa vyema kwenye michuano hiyo kuhifadhi ubingwa huo.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa mwakio amesema kuwa makala hayo yatayavutia zaidi ya mataifa 25 kutoka kote ulimwenguni yaliyoshamiri zaidi kwenye michezo ya martial arts.
Timu ya kenya inatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa mataifa ya Thailand , Phillipines , Iran , Ujerumani miongoni mwa mengine.