Picha kwa Hisani –
Kenya inajiunga na mataifa mengine kote ulimwenguni kuadhimisha siku ya walemavu duniani hii leo.
Siku hii huadhimishwa kwa kujitolea na kutambua haki za watu wenye ulemavu na uwekezaji katika siku zijazo.
Nchini Kenya, Muungano wa walemavu umesema serikali imeweza kuwainua kiuchumi kwa kuwateua katika nyadhfa mbali mbali serikalini, japo kuna vipengelee muhimu vinavyowahusu ambavyo havijahusishwa katika ripoti ya BBI.
Wakati uo huo kundi moja la Wanawake kule Naivasha, kupitia ufadhili wa Obuntu Village, limejitokeza kukomesha unyanyapaa unaoendelezwa na jamii kwa watu wanaoishi na ulemavu wa akili.