Story by Our Correspondents –
Kenya imesema haitatambua uamuzi utakaotolewa Oktoba 12 na Mahakama ya kimataifa ya haki nchini Uholanzi ICJ kuhusu mzozo wa mpaka wa majini baina ya Kenya na taifa la Somalia.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Katibu katika Wizara ya mambo ya nje Balozi Macharia Kamau, imesema Mahakama hiyo ina upendeleo na Kenya imeamua kujiondoa katika kesi hiyo ili kuzuia sintofahamu zaidi.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba uamuzi wa Mahakama hiyo huenda ukachangia mzozo zaidi kwani Kenya imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Somalia lakini katika swala la mipaka ya majini baina ya mataifa hayo mawili haiko tayari kukubali uamuzi wowote.
Wakati uo huo Wizara hiyo imesisitiza kwamba mzozo huo wa mpaka baina ya Kenya na Somalia ni sharti ujadiliwe upya kupitia majadiliano ya kina huku Kenya ikijiunga mataifa mengine yalio wanachama wa umoja wa mataifa kupinga maamuzi yoyote yatakayotolewa na Mahakama hiyo.