Story by Our Correspondents –
Kenya imepokea shehana nyengine ya chanjo ya Corona aina ya Johnson na Johnson yenye dozi 252,000 ili kukabiliana na kikamilifu maambukizi ya virusi vya Corona kote nchini.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupokea shehena hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Mwenyekiti wa jopokazi la linalosimamia chanjo ya Corona Dkt Willis Akhwale amesema kufikia sasa Kenya imepokea dozi 389,600 ya chanjo ya Johnson na Johnson.
Dkt Akhwale amesema serikali imetenga shilingi bilioni 14.3 kusimamia zoezi la kupeyana chanjo ya Corona mwaka kuu pekee ili kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Corona yanapungua kwa asilimia kubwa.
Hata hivyo amewahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi kupokea chanjo ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona huku akidai kwamba kuna baadhi ya kaunti kama ile ya Tana river, Lamu, Bungoma miongoni mwa zengine ambazo wenyeji hawajitokeza jinsi inavyostahili na kupokea chanjo.