Story by Mimuh Mohamed –
Kenya imepokea dozi nyengine milioni 2.2 za chanjo corona aina ya Astrazenaca kutoka taifa la Ujerumani kupitia mpango wa chanjo wa Covax.
Chanjo hiyo ya Astrazeneca imewasili nchini mapema siku ya Alhamis na kupokelewa na maafisa wa Wizara ya Afya nchini wakiongozwa na Mwenyekiti wa jopokazi la kusimamia chanjo dhidi ya Corona nchini Dkt Willis Akhwale.
Chanjo hiyo imewasili wakati ambapo zoezi la kuwachanja wakenya likiwa limeshika kasi katika siku za hivi karibuni, kufuatia onyo la serikali la kuwanyima wakenya huduma muhimu za serikali iwapo hawatakuwa wamechanjwa.
Kulingana na ripoti kutoka kwa Wizara ya Afya nchini kufikia sasa ni watu milioni 7.1 ambao wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya corona humu nchini.