Story by Our Correspondents –
Kenya imepokea dozi 880320 za chanjo aina ya Moderna kutoka taifa la Marekani ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Shehena ya chanjo hiyo imewasili hii leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta na kupokelewa na waalum wa kiafya na wawakilishi wa vitengo mbalimbali vya afya wakiongozwa na Katibu mkuu msimamizi katika Wizara ya afya Dkt Rashid Aman.
Akizungumza baada ya kupokea chanjo hiyo, Dkt Aman ameishukuru serikali ya Marekani kwa kujitolea kuisadia Kenya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Dkt Aman amesema chanjo hiyo aina ya Moderna itasaidia serikali kufikia azma yake ya kuwachanja watu milioni 10 ifikapo mwezi disemba mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurungezi wa kitendo cha kukabiliana na kudhibiti maambukizi kutoka taifa la Marekani Dkt Marc Bulterys amesema Marekani itaendelea kushirikiana na Kenya kufanikisha afya bora kwa wote pamoja kwani imetenga kima cha shilingi milioni 495.
Dkt Marc amedokeza kwamba fedha hizo zitasaidia katika swala la usambazaji wa chanjo, kuwahamasisha wahudumu wa afya, kufuatilia miradi ya afya sawia na kupiga jeki juhudi za kufanikisha afya bora kwa wote.