Picha kwa hisani –
Kenya hii leo imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na ufisadi duniani.
Siku hii huadhimishwa kwa lengo la kuongeza juhudi za kupunguza hatari za ufisadi ulimwenguni na kuhakikisaha mataifa yanakuwa na uwazi katika utendakazi wake.
Katika ujumbe wake kwa ulimwengu, Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres, amesema ufisadi ni uhalifu na usaliti wa amani, hasa wakati huu ambapo ulimwengu unakabiliwa na janga la Corona.
Gutters ameongeza kwamba ujio wa virusi vya corona umeweka wazi kwa ulimwengu kufahamu sehemu ambazo fedha zilizotengwa kupambana na janga hilo zinatumika ipaswavyo ama kwa matumizi ya watu binafsi.
Hapa nchini tume ya maadili na kupambana na ufisadi inaadhimisha siku hii katika hafla inayofanyika kaunti ya Nandi katika uwanja wa kipchoge Keino.