Story by Ephie Harusi –
Kaimu mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa kimatibabu nchini KEMRI, Sam Kariuki amesema Kenya haitakuwa inapokea aina yoyote ya chanjo kutoka kwa taasisi ya GAVI ifikapo mwaka wa 2027.
Kulingana na Kariuki, Kenya haitalazimika kununua chanjo hizo ikiwa taasisi hiyo itajitoa huku akisema serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha inatengeneza chanjo dhidi ya Corona.
Akizungumza na Wanahabari mjini Kilifi, Kariuki amesema hivi karibu wataanza kutengeneza chanjo ya Corona kwa awamu ya kwanza.
Wakati uo huo amesema taasisi ya KEMRI imepata ufadhili wa shilingi milioni 150 kutoka taifa la Uingereza ili kuendeleza utafiti wa ugonjwa wa Corona huku akiongeza kwamba taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanazuia kusambaa kwa virusi ya Corona.