Picha kwa hisani
Rais Uhuru Kenyatta ameonekana kuendeleza siasa za kumkosoa Naibu wake Dkt William Ruto, akisema kuna haja ya viongozi kuungana na kutekeleza majukumu yao ya uongozi.
Rais Kenyatta amemtaka Ruto kuwa na subra katika kuwania kiti cha urais, akisema uongozi haupiganiwi bali hutoka kwa mwenyezi Mungu, huku akizidi kuwahimiza wakenya kushirikiana.
Akihutubia wakaazi wa eneo la Kayole baada ya kufungua rasmi hospitali ya Kayole Level 3 chini mradi wa Serikali, Kiongozi wa taifa amesema ni lazima wakenya waungane pamoja na kujitenga na siasa za vurugu ambazo huvurugu taifa hili.
Rais Kenyatta amewashukuru wawakilishi wa wadi ambao tayari wamepitisha mswada wa BBI katika mabunge yao ya kaunti huku akiwahimiza wakenya kuunga mkono BBI.
Wakati uo huo ameahidi kuwa serikali ina mipango ya kurudisha mradi wa kazi mtaani ili kuhakikisha vijana wananufaika na mradi huo na kuzikabili changamoto za ukosefu wa kazi.