Taarifa na Charo Banda
Malindi, Kenya, Juni 19 – Wadau katika sekta ya kuhifadhi mazingira sasa wanasisitiza haja ya zoezi la upanzi wa miti kuendelezwa hadi ndani ya misitu ya kaya kama njia moja wapo ya kuhifadhi mazingira.
Hii ni baada ya kubainika kwamba asilimia kubwa ya misitu ya kaya kukumbwa na hatari ya kuangamia kutokana na uharibifu unaozidi kuendelea ndani ya misitu hiyo.
Akiongea na wakazi huko eneo la Maindi afisa mkuu wa mazingira katika kaunti ya Kilifi Mariam Jenneby amesema kuwa jumla ya kaya 17 pekee zimesajiliwa rasmi na serikali na kwamba ipo haja ya kaya zote kusajiliwa na serikali na kulindwa kama misitu mingine nchini.
Afisa huyo anasema kuwa ukataji wa miti hivi sasa umeelekezwa kwa misitu ya kaya na kuhatarisha zaidi mazingira, mila na desturi za jamii ya wamijikenda.
Jenneby aidha amesistiza haja ya serikali kupitia maafisa wote wa kulinda misitu, wakazi pamoja na wadau mbali mbali kushirikiana kukomesha uovu huo.