Wizara ya ugatuzi nchini imezitaka kaunti zote 47 nchini kuhusisha wataalam wanapoidhinisha ujenzi wa nyumba katika kaunti zao ili kuhakikisha taifa linakua na miji yenye mpangilio.
Akizungumza katika kongamano la kila mwaka lililoleta pamoja wataalam wa masuala ya ujenzi katika hoteli moja huko Diani kaunti ya Kwale,waziri wa ugatuzi nchini Eugene Wamalwa amesema idadi ya watu inazidi kuongezeka na ni lazima taifa liwe na miji ilionamipangilio.
Wamalwa amesema mipangilio ya miji ikasaidia kumaliza mitaa ya mabanda nchini.