Shinikizo zimetolewa kwa serikali za ugatuzi Pwani kubuni sera na sheria maalum zitakazotumia kutoa muuongozi utakaofanikisha usawa wa walemavu katika afisi za kiserikali.
akiongea mjini mombasa mkurugenzi wa shirika la kijamii linaloangazia maswla ya walemavu la Wezesha Community Organization Vincent Macmbinji ametaja kuwa idadi ya walemavu ni ndogo mno kwenye afisi za kiserikali hatua aliyoitaja kama unyanyasaji na uwakilishi duni dhidi yao.
mkurugenzi huyo aidha ameongezea kwamba afisi nyingi za kiserikali pwani zimekiuka sheria ya katiba kuwa kila afisi ya kiserikali inapaswa kuwa na asilimia 5 ya watu wanaoishi na ulemavu.
Amesema kuwa walemavu wamehitumi kwenye taaluma mbalimbali hivyo basi kuana haja ya walemavu kutambuliwa kama wakenya wengi.
Taarifa na Hussein Mdune.