Story by Our Correspondents-
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imetangaza rasmi kwamba uchaguzi wa ugavana katika kaunti za Mombasa na Kakamega utaandaliwa tarehe 29 mwezi huu.
Katika kikao na wagombea wa kaunti hizo, Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema hakuna changamoto zozote zitakazoshuhudiwa katika kaunti hizo huku akidokeza kwamba wagombea hao wana mda wa kufanya kampeni zao hadi tarehe 27.
Chebukati pamoja na makanishna wote wa IEBC wamehudhuria kikao hicho na kuwataka viongozi hao kuhakikisha wanazingatia kaunti zote za tume ya IEBC katika kufanya kampeni zao hadi siku ya mwisho ya uchaguzi huo.
Kwa upande wake Afisa mkuu mtendaji wa IEBC Marjan Hussein Marjan amewahakikishia wagombea wote wa uchaguzi huo kwamba maandalizi yamekamilika na hakuna changamoto zozote zitakazoshudiwa.
Hata hivyo wagombea hao wamekubaliana na msimamo wa IEBC na kuahidi kufanya kampeni zao kwa kuzingatia kanuni za IEBC sawa na kuafikiana kutumia majenti wao wa awali kuwawakilisha katika uchaguzi huo.