Picha kwa Hisani
Gavana wa kaunti ya Tana river Meja mstaafu Dhadho Godhana ameitaka Serikali kuu kusambaza fedha kwa serikali za kaunti ili kuziwezesha kaunti kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wakenya mashinani.
Godhana amesema kaunti ya Tana river haijapokea kima cha shilingi milioni 550 cha mwezi Juni hali inayoifanya Serikali ya kaunti hiyo kushindwa kuweka mipangilio inayostahili katika kuzuia virusi vya Corona.
Godhana amesema Serikali ya kaunti hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi katika kulipa madeni yake kutokana na kucheleweshwa kwa fedha hizo, akiitaka Serikali kuu kuzituma fedha hizo mashinani.
Wakati uo huo, Godhana amepinga vikali mabadiliko katika mfumo wa ugavi wa fedha kwa serikali za kaunti ambao umezua malumbano makali katika bunge la Seneti.