Mradi wa kunyunyiza dawa maeneo mbalimbali ya kaunti ya Mombasa kwa kutumia mtambo maalum wa Drone utasaidia katika kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa wakaazi wa kaunti hiyo.
Mshirikishi mkuu wa Shirika la Msalaba mwekundu kaunti ya Mombasa Mohammed Rajab amesema mradi huo ni wa kipekee na unalenga kupunguza maambukizi hasa katika maeneo yaliyo na shughuli nyingi.
Akizungumza kule Mombasa, Rajab amesema mtambo huo ambao utapepea angani na kunyunyiza dawa maeneo mbalimbali, utapunguza athari za watu wanaozuru maeneo hayo kuambukizwa virusi vya Corona.
Wakati uo huo amefichua kuwa mtambo huo hautawapulizia watu dawa hiyo aina ya ‘Chlorine’ bali utayapulizia maeneo nyakati za usiku ili watu wanaozuru maeneo hayo wasiwekwe katika hatari ya maambukizi.