Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amesema jamii inafaa kushirikiana kikamilifu na serikali, iwapo inalenga kulikabili tatizo la ugaidi na misimamo mikali katika eneo la Pwani.
Akihutubu kwenye Kongamano lililowaleta pamoja vijana kujadili mbinu mwafaka za kukabiliana na ugaidi mjini Mombasa, Joho amesema ni sharti kila mmoja ajitolee kikamilifu kupiga vita swala la ugaidi.
Aidha amesema kuna haja ya kila mmoja kuwa mstari wa mbele katika harakati za kufanikisha vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali miongoni mwa jamii.
Kwa upande wake Kamishna wa Mombasa Evans Achoki amesema vijana wana mchango mkubwa katika kupiga vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali ili kuimarisha uchumi wa taifa na kuwepo na usalama dhabiti.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.