Story by Gabriel Mwaganjoni:
Serikali ya kaunti ya Mombasa imehimizwa kuweka wazi takwimu zake na mipangilio ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wakaazi wa kaunti hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la LENGO Lucas Fondo amesema ni kupitia takwimu hizo ndipo Serikali ya kaunti hiyo itakuwa na uwezo wa kuweka mipangilio yake kuambatana na matakwa ya wakaazi.
Fondo amesema Serikali ya kaunti ya Mombasa imekosa mipangilio kwa wakaazi kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika idara mbalimbali za serikali ya kaunti hiyo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuzindua mradi wa ushirikiano kati ya Shirika hilo na Serikali ya kaunti ya Mombasa katika kukusanya takwimu kwa ajili ya maendeleo ya kaunti, Fondo ameitaka Serikali ya kaunti ya Mombasa kuwajibika.