Katika juhudi za kukomesha dhuluma za kijinsia katika mazingira ya kazi, sasa serikali ya Kaunti ya Mombasa imeidhinisha mikakati ya kuwahamasisha wafanyikazi wake kuhusiana na swala hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya jinsia katika Kaunti hiyo Bi Esther Ingolo amesema hamasa hizo ni muhimu kwani zitawawezesha wafanyikazi hao kutambua haki zao katika mazingira ya kazi na kuchukua hatua mwafaka za kisheria kupigana na dhuluma za kijinsia.
Akizungumza katika mkao wa hamasa kwa Wafanyikazi wa Kaunti kuhusu dhuluma za jinsia Mjini Mombasa, Bi Ingolo amesema kwamba swala la dhuluma za kingono hasa katika mazingira ya kazi ni swala ambalo limeangaziwa katika majadiliano hayo.
Bi Ingilo hata hivyo anasisitiza kwamba vikao hivyo vya hamasa vitaimarishwa kwani ni bayana visa hivyo hutendeka japo ni wachache wanaochukua sheria dhidi ya wahalifu hao.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.