Kitengo cha kukabiliana na maradhi ya kifua kikuu na ukoma katika Kaunti ya Mombasa sasa kimezindua mbinu ya kuzuru mashinani ili kuwakagua, kuwapima na kuwaanzishia tiba wagonjwa wa TB.
Afisa mkuu wa kitengo hicho katika Kaunti ya Mombasa Daktari Samson Kioko amesema kwamba hatua hiyo imetokana na kupungua kwa watu wanaofika katika hospitali za umma ili kupimwa ugonjwa huo licha ya kukohoa mfululizo.
Kioko amesema kwamba ukosefu wa lishe bora miongoni mwa Wakaazi wa Kaunti hiyo hasa wanaume umepeleka maambukizi hayo na akaisihi jamii ya Kaunti hiyo kubadili mienendo yao ya kula.
Mtaalam huyo anawataka wakaazi kubaini ishara za maradhi hayo kama vile mgonjwa kutokwa na jasho jingi wakati wote, kukosa hamu ya chakula, kukohoa mfululizo, kutapika damu au kupunguza uzani ili wapimwe na kutibiwa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.