Serikali ya kaunti ya Mombasa imeshikilia msimamo wake kuwa baada ya muda wa siku 21 ilizotoa kwa wamiliki wa majumba katika kaunti hiyo kuwasilisha stakabadhi zao za ujenzi kwa idara husika, kukamilika pasi na stakabadhi zozote basi majengo yao yatabomolewa.
Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amesema serikali ya kaunti hiyo itahakikisha majumba yote yaliojengwa yanaambatana na sheria na kanuni za ujenzi katika kaunti hiyo.
Amesema mda huo wa siku 21 unalenga kuwapa fursa wamiliki hao ambao walijenga bila ya kuidhinishwa na serikali ya kaunti ya Mombasa ili kuhakikisha wanawasilisha stakabadhi zao kwa idara husika.
Joho amefichua kuwa mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo basi nyumba yake itaidhinishwa kama jengo lililojengwa mahali pasipofaa na kubomolewa.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.