Waziri wa mazingira kaunti ya Mombasa Godfrey Nato amesema kaunti ya Mombasa itaekeza zaidi katika harakati za kutatua tatizo la mirundiko ya taka katika kaunti hiyo.
Nato amesema majaa ya taka katika kaunti hiyo yamesababisha mvutano kati ya serikali ya kaunti ya Mombasa na mamlaka ya safari za ndege nchini, kuhusu swala la usalama wa safari za ndege kwenye maeneo yenye majaa ya taka.
Nato hata hivyo amesisitiza kuwa swala la usafi wa mazingira sio jukumu la serikali ya kaunti pekee bali pia wakaazi wa kaunti ya Mombasa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.