Story by Gabriel Mwaganjoni –
Serikali ya kaunti ya Mombasa imeimarisha mchakato wake wa kuihamasisha jamii ya kaunti hiyo kuhsu afya ya uzazi.
Afisa mkuu wa afya katika kaunti hiyo Pauline Oginga amesema juhudi hizo zinatokana na changamoto nyingi zinazokumba afya ya uzazi kwa jamii hasa jinsia ya kike.
Akizungumza alipozindua huduma tamba za afya ya uzazi, Pauline amehoji kuwa wakaazi wamekuwa wakikimbilia huduma za maduka ya dawa ili kujinunulia dawa bila ya muongozo wa watalaam wa afya.
Msaada huo wa kliniki tamba ya afya ya uzazi kulingana na Pauline ni afueni katika juhudi za kuimarisha afya ya uzazi miongoni mwa wakaazi wa kaunti hiyo.