Story by Mwanaamina Fakii –
Kamati ya dharura ya kudhibiti virusi vya Corona katika kaunti ya Kwale, imetoa tahadhari ya ongezeko la maambuzi ya virusi vya Corona.
Katika kikao na Wanahabari katika majengo ya bunge la kaunti ya Kwale, Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya nchini umebaini kwamba watu wawili wameambikizwa virusu vya Corona ndani ya saa 24 zilizopita.
Mvurya amesema wagonjwa wengine tisa wametengwa katika hospitali ya rufaa ya Msambweni huku wengine watatu wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.
Kwa upande wake Kamishna wa Kwale Joseph Kanyiri, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuzingatia masharti ya kudhibiti Corona huku akisema maafisa wa usalama watakabiliana kikamilifu na wale watakaokiuka masharti hayo.