Story by Janet Shume –
Kaunti ya Kwale imetajwa kuwa miongoni mwa kaunti za Pwani zinazokabiliwa na changamoto ya ulanguzi wa binadamu huku walengwa wakiwa vijana na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika linalopambana na ulanguzi wa binadamu la Peace Tree Network Martha Okumu amesema utafiti uliyofanya umeonyesha wazi kwamba maeneo ya fuo za bahari hindi ni kati ya maeneo yanayotumiwa kuendeleza visa hivyo.
Akizungumza katika kongamano la siku tatu lililoandaliwa katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale la kuangazia jinsi ya kudhibiti visa hivyo, Martha amesema ni lazima visa vya ulanguzi wa binadamu vikabiliwe.
Martha amesema Kongamano hilo linalenga kutoa mafunzo kwa wakaazi kuhusu jinsi wanavyoweza kuepuka mitego ya walanguzi hao.