Mwakilishi wa wadi ya Macknon katika bunge la kaunti ya Kwale Joseph Danda, anaishauri serikali ya kaunti ya Kwale kuanzisha miradi zaidi ya uchimbaji mabwawa katika sehemu za mashinani, ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji.
Danda, anasema wakaazi wengi wa mashinani wanateseka na tatizo la uhaba wa maji na akautaka uongozi wa kaunti kutilia maanani pendekezo lake kwauharaka.
Danda ameeleza kuwa kuwa wakaazi wengi wa mashinani hulazimika kusafiri mwendo mrefu kutafuta bidhaa hiyo muhimu, akisisitiza kuwa hatua hiyo itasadia pakubwa kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji.
Taarifa na Cyrus Ngonyo