Story by Hussein Mdune-
Naibu gavana wa kaunti ya Kwale Chirema Kombo amesema kuna haja ya wahisani kujitokeza na kuwasaidia wahanga wa njaa na chakula ikiwemo shule ambazo zinakabiliwa na kiangazi kikali katika kaunti hiyo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupokea chakula cha msaada kutoka kwa Wakfu wa Rashid Abdillah Supercup, Kombo amesema wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani yao ya kitaifa wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa chakula.
Kombo amesema chakula hicho kitasambazwa kwa wakaazi ambao wameathirika na baa la njaa hasa maeneo ya Kinango na LungaLunga.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Wakfu wa Rashid Abdallah Supercup Luiza Kithi ameahidi kushirikiana na kaunti ya Kwale kuhakikisha familia zilizoathirika na baa la njaa zinasaidika.
Bidhaa ambazo kaunti ya Kwale imepokea kutoka kwa wakfu huo ni pamoja na Unga wa Mahindi, Mafuta ya kupikia, Maharagwe, majani chai, Mchele miongoni mwa bidhaa zingine.