Story by Janet Shume
Wizara ya elimu katika serikali ya kaunti ya Kwale imeeleza kutoridhishwa na matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KSCE ya mwaka wa 2021 ya wanafunzi waliofadhiliwa kimasomo na serikali ya kaunti hiyo.
Katibu katika wizara hiyo Juma Nzao amesema ni wanafunzi 44 pekee waliopata alama ya A na A- kati ya wanafunzi 692 waliokuwa katika mradi wa ufadhili wa masomo unaoendelezwa na serikali ya kaunti hiyo.
Akizungumza na Wanahabari, Nzao amesema hali hiyo imechangiwa pakubwa na hatua ya wanafunzi wanaopata ufadhili huo kutotia bidii masomoni.