Serikali ya kaunti ya Kwale imeahidi kuzidisha juhudi zaidi za kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona katika kaunti hiyo.
Gavana wa Kwale Salim Mvurya, amesema wameafikia na wadau wa kiusalama kuweka vizuia katika maeneo ya mipakani hasa katika sehemu za Bonje, Sunza, Kilibasi, Kiteje, Jasini, Vanga na mpaka wa Kenya na Tanzania.
Mvurya amesema wamebaini kuwa watu wanatumia njai za mkato katika sehemu hizo kuingia na kutoka katika kaunti hiyo hali ambayo ni hatari zaidi dhidi ya maambukizi hayo.
Wakati uo huo amedokeza kuwa tayari watu 16 ambao waliingia kaunti ya Kwale kutoka taifa jirani la Tanzania wameekwa Karantini, akisema mpango wa kuwafanyia vipimo vya Corona wakaazi wa Kwale unaendelea japo changamoto ni ukosefu wa vifaa hitajika.