Story by Salim Mwakazi –
Serikali ya kaunti ya Kwale inalenga kukusanya ushuru wa zaidi wa shilingi milioni 275 katika mwaka wa kifedha wa 2021/2022.
Waziri wa fedha katika serikali ya kaunti ya Kwale Bakari Sebe amesema ili serikali hiyo iafikie fedha hizo italazimika kuongeza kiwango cha ushuru katika bajeti ya ziada na itategemea ukuaji wa uchumi wa taifa.
Akizungumza na Wanahabari, Sebe amesema licha ya taifa kukabiliwa na changamoto za janga la Corona ni lazima mahitaji ya serikali ya kaunti hiyo yatekelezwe.
Wakati uo huo amedokeza kuwa kupungua kwa kiwango cha ushuru kutaathiri pakubwa matumizi ya serikali na miradi ya maendeleo ya kaunti hiyo ndiposa serikali ya kaunti imeandaa mikakati muafaka ya kuhakikisha inaafikia matumizi yake.