Story by Janet Shume –
Wazazi wa wanafunzi waliomaliza darasa la nane katika kaunti ya Kwale wametakiwa kutembelea afisi za wasimamizi wa wadi katika maeneo yao ili kuanza mipangilio ya mapema ya kupata ufadhili wa karo za watoto wao.
Waziri wa elimu katika serikali ya kaunti ya Kwale Mangale Chiforomodo amesema serikali ya kaunti hiyo tayari imetenga fedha za kugharamia masomo ya shule za upili kwa wanafunzi hao ili kuhakikisha wanaendelea na masomo yao bila changamoto.
Choforomodo amesema wizara hiyo imeanza kunua vifaa vya kupima kiwango cha joto mwilini vitakavyosambazwa katika shule za chekechea kwa lengo la kufuatilia na kuwakinga wanafunzi na maambukizi ya virusi vya Corona.