Serikali ya kaunti ya Kwale imefikisha idadi ya vitanda 300 vinavyohitajika na serikali kwa kila kaunti hasa vya kulazwa kwa wagonjwa wa virusi vya Corona.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuitembelea hospitali ya rufaa ya Msambweni, Naibu Gavana wa Kwale Bi Fatuma Achani, amesema tayari jumla ya vitanda 290 na kupitisha idadi ya vitanda vinavyohitajika kwa tayari kaunti hiyo ilikuwa na vitanda 100.
Achani ameweka wazi kuwa vitanda 84 vitasalia katika hospitali ya Msambweni huku vingine vikisambazwa katika hospitali zingine za kaunti hiyo.
Wakati uo huo amedokeza kuwa mwafaka ya kukabiliana na changamoto za nguvu za umeme katika hospitali ya Rufaa ya Msambweni umetatuliwa baada ya serikali ya kaunti hiyo kununua jenereta.