Picha kwa hisani –
Serikali ya kaunti ya Kwale imesema kwamba uhaba wa dawa za kutibu ugonjwa wa Malaria katika hospitali za kaunti hiyo umechangiwa na hatua ya serikali ya kitaifa kukosa kusambaza dawa hizo kwa kaunti hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya Afya katika bunge la kaunti ya Kwale Mwinyi Mwasera amsema ni zaidi ya miezi mitatu sasa serikali ya kitaifa imekosa kusambaza dawa katika hospitali za kaunti .
Mwasera amepinga madai kuwa hospitali na zahati za kaunti hiyo hazina dawa za kutibu magonjwa mengine, akisema madai hayo hayana msingi.