Picha kwa Hisani –
Mshirikishi wa kitengo cha lishe bora kaunti ya Kilifi Ronald Mbunya amesema Kaunti hio inaongoza kwa idadi ya watoto waliodumaa .
Akizungumza na wanahabari Mbunya amesema utafiti uliofanywa mwaka wa 2014 umeonyesha kuwa asilimia 31 ya watoto katika kaunti hiyo ya kilifi hawapati lishe bora.
Mbunya ameyataja maeneo ya Ganze na Magarini kuwa miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na tatizo la watoto kudumaa.
Mbunya ameongeza kwamba watoto wanaozaliwa na wanawake waliona umri mdogo pamoja na wale wanoishi na virusi vya Ukimwi wako kwenye hatari zaidi ya kudumaa.
Hata hivyo ameitaka serikali ya kitaifa na ile ya Kaunti ya kilifi kuwapa msaada wa kifedha waakazi ambao watoto wao wameathirika kiafya kufuatia ukosefu wa lishe bora ili waweze kujikimu