Picha kwa hisani –
Kamati ya usalama pamoja na Serikali ya kaunti ya Kilifi, sasa imeweka wazi kuwa maambukizi ya virusi vya Corona yameanza kuchipuka upya katika kaunti ya Kilifi licha ya Serikali kusisitiza wakenya kuzingatia masharti ya Covid 19.
Akizungumza mjini Kilifi katika kikao na maafisa wa usalama, Gavana wa Kilifi Amason Jefwa Kingi amesema jumla ya visa vinane vimeripotiwa katika muda wa siku moja pekee hali ambayo imeleta wasiwasi miongoni mwa wakaazi.
Kingi anasema hatua ya wakazi kutozingatia masharti ya kiafya hasa katika mikusanyiko ya watu ndio imechangia pakubwa visa vya Corona kuchipuka upya katika kaunti hiyo.
Kwa upande wake Kamishna wa kaunti hiyo Kutswa Olaka amesistiza haja ya kila mmoja kuzingatia kanuni za wizara ya afya ili kuepuka maambukizi ya Corona huku akionya kuwa atakayekiuka masharti hayo atachukuliwa sheria.