Waziri wa Elimu katika Serikali ya kaunti ya Kilifi Profesa Gabriel Katana, amesema kaunti ya Kilifi ina upungufu wa takriban walimu 2,400.
Profesa Katana amesema changamoto hiyo ndio iliyopelekea shule kuorodhesha matokeo duni katika mitihani ya kitaifa.
Waziri huyo wa Elimu amewataka viongozi wa kisiasa kuingilia kati swala hilo na kuliwasilisha mbele ya Tume ya kuajiri walimu nchini TSC ili walimu zaidi kuongezwa katika kaunti hiyo.
Kauli ya Waziri huyo inajiri huku wanafunzi wengi waliosajiliwa kujiunga na kidato cha kwanza wakianza kuripoti rasmi katika shule walizoitwa.
Taarifa na Hussein Mdune.