Story by Charo Banda-
Serikali ya kaunti ya Kilifi imetangaza kwamba itayabomoa majengo yote yaliojengwa kwa njia haramu katika ardhi inayomilikiwa na hospitali ya Mariakani.
Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi amesema serikali ya Kilifi kupitia Wizara ya ardhi imeafikia uamuzi huo kutokana ongezeko la unyakuzi wa ardhi za taasisi za afya katika kaunti hiyo.
Kingi amehoji kuwa ni lazima ardhi za taasisi za umma zilindwe dhidi ya wanyakuzi wa ardhi, akishikilia kuwa hatua ya serikali ya kaunti hiyo kuyabomoa majengo yaliojengwa kwa njia za kilaghai lazima itatekelezwa.
Kwa upande wao wakaazi wa eneo la Mariakani wameishabikia hatua hiyo wakiitaka serikai ya kaunti ya Kilifi kusimama kidete na kuhakikisha ardhi ya hospitali ya Mariakani ilionyakuliwa inarejeshwa chini ya hospitali hiyo.