Story by Charo Banda-
Serikali ya kaunti ya Kilifi imeweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha inafufua sekta ya utalii baada ya kuonekana kusambaratika kutokana na janga la Corona.
Gavana wa kaunti hiyo Amason Jefwa Kingi amesema Kenya imeirodheshwa kuwa sio salama kutokana na kunakiliwa kwa idadi ya juu ya virusi vya Corona.
Akizungumza katika kaunti hiyo baada ya uzinduzi wa chanjo ya Corona aina ya Mordana kwa wahudumu wote wa sekta ya utalii kaunti ya Kilifi, Gavana Kingi amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha uchumi na kuhakikisha watalii wako usalama.
Kwa upande wake Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali ya Malindi Emily Karisa amesema wanalenga kuwachanja zaidi ya wahudumu 300 wa sekya ya Utalii ili kuhakikisha usalama wa watalii wanaolenga kuzuru kaunti hiyo wako salama.
Hata hivyo baadhi ya wahudumu wa sekta ya utalii waliojitokeza kupokea chanjo hiyo wameunga mkono mpango huo, wakisema utaimarisha zaidi sekta ya Utalii.