Story by Ephie Harusi –
Msimamizi mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kujikinga na kuboresha afya kaunti ya Kilifi Daktari Ummi Bunu amesema Idara ya afya katika kaunti hiyo wameweka mikakati ya kuhakikisha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kinapungua.
Kulingana na Daktari Ummi, eneo la Kilifi kusini, Kaloleni na Ganze ni miongoni mwa maeneo yaliothirika pakubwa na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Akizungumza na Wanahabari, Daktari Ummi amesema maafisa wa afya wamekuwa wakiendeleza hamasa mashinani kuhusu jinsi wakaazi wanavyoweza kujikinga na mambukizi ya Malaria.
Wakati uo huo amesema wanawake wajawazito ni miongoni mwa wale wanaoathirika pakubwa na ungojwa wa Malaria, akiwataka wakaazi kutumia vyandarua vya kuzuia mbu.