Story by Ephie Harusi –
Naibu Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Saburi amesema serikali ya kaunti hiyo imeweka mikakati ya kuongeza pesa za kupambana na ugonjwa wa ukimwi katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022.
Saburi amesema kima cha shilingi milioni 4 ambacho serikali ya kaunti hiyo inatoa kila mwaka hakiwezi kukidhi mahitaji ya wagonjwa ambao wameathirika na virusi vya Ukimwi.
Akizungumza mjini Kilifi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, Saburi amesema serikali ya kaunti ya Kilifi itakuwa inawapa waathiriwa wa ugonjwa huo pesa kila mwezi za kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake Afisa wa afya ya umma katika kaunti ya Kilifi Erick Maitha amesema takwimu zilizofanywa zimeonyesha kwamba wanawake wanaongoza kwa idadi maambukizi ya HIV ikilinganishwa na wanaume katika kaunti ya hiyo.