Story by Our Correspondents
Kauli za kusameheana zimerindima katika halfa ya 19 ya maombi ya kitaifa yaliandaliwa katika hoteli ya Safari Park jijini Nairobi huku viongozi wa kidini wakichukua jukumu la kuhimiza umuhimu wa kusameheana.
Akihutubia wakenya wakati wa halfa hiyo, Rais Uhuru Kenyatta amesema taifa hili litashuhudia amani iwapo wakenya na viongozi mbalimbali wataungana na kuzidi maombi huku akihimiza kila mmoja kuwa balozi wa amani.
Naye Naibu Rais Dkt William Ruto aliyehudhuria halfa hiyo amemuomba msamaha Rais Kenyatta kutokana na tofuati zao za kisiasa huku akiahidi kuwasamehe wale wote waliotofautiana katika njia moja ua nyengine ili taifa hili lishuhudie uchaguzi wa amani.
Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa la kianglikana nchini Jackson Ole Sapit amewasihi wakenya kusameheana na kuishi kwa upendo kwa ajili ya mshikamano wa taifa hili.
Hata hivyo Askofu mkuu wa Kanisa la Katoliki jimbo la Nyeri, Antony Muheria amewataka wakenya kuzidisha maombi ili taifa hili lisonge mbele kimaendeleo sawa na kushuhudiwa kwa uchaguzi huru na haki.