Picha kwa hisani –
Huku maadhimisho ya miaka kumi ya katiba ya mwaka 2010 yakiendelea nchini Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema taifa lilikua na safari ndefu kabla ya kupata katiba hio mpya.
Katika kikao na wanahabari Odinga amesema kwamba safari ya Kenya kupata katiba mpya ilipelekea baadhi wakenya kupitia mateso wengine wakiuwawa na kwamba katiba ya nchini infaa kuheshimiwa.
Naye kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi amesema kabla ya katiba ya nchini kufanyiwa mabadiliko lazima kufanywe utathimini wa kina kuhusu katiba hio kabla ya baadhi ya vipengele kufanyiwa mabadiliko.
Mudavadi amesema mchakato wa kufanyia marekebisho katiba ya nchini kupitia ripoti ya BBI una msukumo wa kisiasa akisema baadhi ya vipengele vya katiba havijatekelezwa ipasavyo ikiwemo kipengele cha tuluthi mbili ya usawa wa kijinsia.