Picha kwa Hisani –
Huku katiba ya sasa ikitarajiwa kufikisha mwongo mmoja tangu ilipopitishwa ifikapo siku ya alhamisi juma hili,jaji mkuu nchini David Maraga amesema hajaridhishwa na jinsi katiba hio inavyotekelezwa.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Maraga amesema katiba ya kenya ni katiba bora zaidi ikilinganishwa na zile za mataifa mengine ulimwenguni lakini viongozi walioko mamlakani wamekosa kuitekeleza inavyostahili.
Naye mtetezi wa haki za kibinadam kutoka shirika la Haki Afrika Hussein Khalid ametoa kauli sawa na hio akisema katiba haijatekelezwa vilivo kwani licha ya baadhi ya vipengele kuangazia suala la ardhi wakaazi wa pwani bado wameendelea kunyanyaswa katika ardhi zao.
Katiba ya sasa ilipitishwa tarehe 27 mwezi agosti mwaka 2010 na ifikapo tarehe 27 mwezi huu wa agosti mwaka 2020 yaani siku ya alhamisi juma hili katiba hio itafikisha miaka 10 tangu kuidhinishwa rasmi.