Picha kwa hisani –
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amemteua tena mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, kuendelea na wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Asubuhi ya leo mpambe wa rais Magufuli amewasilisha bahasha ambayo ilikuwa na jina la Majaliwa ili kusomwa bungeni.
Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Magufuli uliokamilika mwezi uliopita.
Waziri Mkuu huyo mteule sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge kwa kupigiwa kura, na jina lake likipita bungeni ataapishwa rasmi kushika wadhifa huo.