Story by Mimuh Mohamed-
Kinara wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amekosoa hatua ya baadhi ya wanasiasa ya kuendeleza siasa za vurugu kwa kutatiza mikutano ya wapinzani wao.
Akizungumza na Wanahabari Karua amewataka wakenya kujitenga na siasa za vitisho na vurugu akisema kila mwanasiasa anapaswa kuuza sera zake pasi na kutatiza mikutano ya wapinzani wake.
Karua amesema kwa jinsi hali ilivyo kwa sasa ambapo mikutano ya kisiasa inashughudia vurugu ni wazi baadhi ya wanasiasa wanatumia vibaya wakenya katika kuzua rabsha.
Kauli ya Karua imejiri baada ya tukio la siku ya Jumamosi katika kaunti ya Meru ambapo hotuba ya mke wa kiongozi wa ODM Raila Odinga, Bi Ida Odinga ilitatizwa na kundi la watu waliohudhuria mkutano huo.