Story by Hussein Mdune –
Kinara wa Chama cha Narc Kenya Martha Karua ametangaza rasmi kujiunga na Muungano wa Azimio la umoja ili kumpigia debe Odinga katika azma yake ya kuwania kiti cha urais mwezi Agosti 9.
Karua amesema taifa la Kenya linahitaji kiongozi wenye malengo ya kuwanufaisha wakenya wote na wala sio kiongozi wenye fikra binafsi huku akishikilia kwamba huu ndio wakati mwafaka wa taifa la Kenya kushuhudia mabadiliko.
Akizungumza katika kikao cha pamoja na viongozi wa chama cha ODM na Narc Kenya kule jijini Nairobi, Karua amesema viongozi hao wawili wamekuwa wakishirikiana kwa maswala mbalimbali kwa mda mrefu.
Kwa upande wake Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga anawania kiti cha urais kupitia Muungano wa Azimio la umoja, amesifu hatua ya Karua ya kujiunga na Muungano wa azimio akisema watashirikiana kuhakikisha wanafanikisha maendeleo.
Hata hivyo Katibu mkuu wa Chama cha Narc Kenya Michael Orwa ameweka wazi kwamba chama cha Narc Kenya kimejiondoa rasmi katika Muungano wa OKA na kujiunga na Azimio la umoja.