Story by Salim Mwakazi –
Kamishna wa kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kususia mikutano ya kisiasa ili kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kanyiri amesema mikutano ya kisiasa imechangia ongezeko la maambukizi ya Corona katika kaunti ya Kwale kutokana na idadi kubwa wakaazi kupuuza masharti ya kudhibiti maambukizi hayo na kushabikia siasa.
Akizungumza na Wanahabari, Kanyiri amesema ni lazima kila mkaazi kuzingatia masharti ya kudhibiti Corona hasa kuvaa barakoa, kuosha mikono kila mara, kuzingatia umbali wa mita moja na kujitenga na mikusanyiko ya watu.
Kauli yake imejiri baada ya hospitali ya rufaa ya Msambweni kuripotiwa kuzidiwa na uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa wa Covid-19.